1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken: Wagner inatumia mapinduzi ya Niger kwa manufaa yake

8 Agosti 2023

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametahadharisha kwamba mamluki wa kundi la Wagner la Urusi wanaitumia hali ya kukosekana utulivu nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4UvI2
Belarus | Wapiganaji wa Wagner
Wapiganaji wa kundi la Wagner wakifanya mazoezi BelarusPicha: Voen Tv/Belarusian Defence Ministry/Handout/REUTERS

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametahadharisha kwamba mamluki wa kundi la Wagner la Urusiwanaitumia hali ya kukosekana utulivu nchini Niger, ambayo jirani yake Mali ni mshirika wa Urusi.

Waziri huyo wa Marekani amesema anaamini kwamba kilichotokea na kinachoendelea nchini Niger hakikuchochewa na Urusi wala na mamluki wa kundi la Wagner, hata hivyo ameeleza kuwa mamluki hao wanajaribu kuitumia hali iliyotukia nchini humo. Blinken amesema popote pale ambapo wapiganaji hao wamekwenda wamesababisha vifo, uharibifu na unyonyaji.