1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blechschmidt aachiwa huru Afghanistan

Heinzle/Oummilkheir11 Oktoba 2007

Baada ya kuachiwa huru mhandisi wa kijerumani Rudolf Blechschmidt aliyeshikiliwa mateka kwa muda wa wiki 12 nchini Afghanistan,familia yake inataraji atarejea nyumbani haraka.

https://p.dw.com/p/C77r
Rudolph Blechschmidt kabla ya kuachiwa huru
Rudolph Blechschmidt kabla ya kuachiwa huruPicha: AP

”Mpaka dakika hii hatuamini kama kweli kaachiwa huru”-amesema hayo mwanawe wa kiume Markus,mbele ya waandishi habari.Pengine leo hii Rudolf Blechschmidt atawasili nchini Ujerumani.

Si magari mengi yanayopita karibu na ubalozi wa Ujerumani katika eneo la kati la mji mkuu Kabul.Na hakuna yeyote aliyetambuqa,pale gari iliyokua ikimsafirisha Rudolf Blechschmidt ilipoingia katika uwanja wa ubalozi huo,saa moja kasoro daakika ishirini za usiku,jana.Hapo tena milango ya kuingia katika jingo hilo la ubalozi linalolindwa kupita kiasi,ikafungwa.Blechschmidt hakutaka kuonana na waandishi habari na wapiga picha,baada ya kuachiwa huru.Mara baada ya kuwasili mhandisi huyo mwenye umri wa miaka 62 alichcunguzwa na timu ya madaktari wa jeshi la shirikisho Bundeswehr.Amekonda kweli kweli,lakini afya yake inaonyesha kua nzuri.

Baadae akazungumza kwa simu na familia yake nchini Ujerumani na kula chakula cha usiku katika ubalozi wa Ujerumani ambako pia ndiko alikolala.

Muadhini alipoanza kuwahimiza watu wakasali na kufuturu,kama ilivyo kawaida kwa waislam katika mwezi kama huu wa ramadhan,Rudolf Blechschmidt alikua tayari keshaachiwa huru,na yuko njiani kuelekea mjini Kabul.

Harakati za kuachiwa kwake huru zilikamilika kabla ya magharibi kuingia.Utaratibu mzima uligubikwa na patashika.Wateka nyara walikua na wasi wasi kupita kiasi.Walihofia mambo yasije yakenda kombo kama ilivyotokea wiki mbili zilizopita,pale baadhi ya wafuasi wao walipokamatwa hata kabla ya Blechschmidt kuachiwa huru.Wakati ule eateka nyara wakawakamata upya Blechschmidt na wenzake wanne wa kienyeji.Safari hii lakini mambo yalikwenda kama ilivyopangwa.

Kiongozi wa mkoa wa Yaghatu,umbali wa kilomita mia moja kusini mwa mji mkuu Kabul,akidhibitisha kwamba Blechschmidt ameachiwa huru muda mfupi kabla ya saa kumi na moja jioni na kwamba ameshawasili katika eneo salama mkoani humo.Badala yake serikali ya Afghanistan imewaachia huru wafungwa watano,wanaharakati wa kundi lililomteka nyara Blechschmidt na wenzake,akiwemo pia baba wa kiongozi wa wateka nyara Mullah Nizamuddin.Hakuna aliyetaka kusema kama fedha zimetolewa ili Blechschmidt aachiwe huru.Lakini kila mmoja anaamini fedha zimelipwa tuu seuze tena,hilo ndilo suala kubwa lililoingia midomoni tangfu wiki kadhaa sasa.Lakini hata kuachiwa huru wanaharakati wa kundi hilo pengine ndio chanzo cha kuachiwa huru Blechschmidt na wenzake.Amri imetoka juu kabisa,imetoka kwa rais Hamid Karzai mwenyewe.

Kwa mara nyengine tena madai ya wateka nyara yameitikwa-kama ilivyotokea katika kesi za mahabusi kadhaa wa kigeni nchini Afghanistan.Kwa mara nyengine tena hatima ya mahabusi imepewa umbele badala ya msimamo mkali dhidi ya weateka nyara.Kwa namna hiyo wateka nyara watazidi kupata nguvu,kama wanavyosema wadadisi mjini Kabul.Si hasha kufumba na kufumbua tukasikia na wengine pia wametekwa nyara.

Rudolf Blechschmidt amesaaklimika baada ya kushikiliwa mateka kwa muda wa wiki 12.Haijulikani lakini kama atarejea nyumbani,wala lini.