Blatter: ubaguzi lazima uangamizwe | Michezo | DW | 02.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Blatter: ubaguzi lazima uangamizwe

Rais wa FIFA Sepp Blatter ameleezea wasiwasi wake kuhusiana na ripoti inayoonesha kiwango cha tatizo la ubaguzi wa rangi katika kandanda la Urusi, kabla ya Kombe la Dunia la mwaka wa 2018

Blatter ameonya kuwa “lazima hatua kadhaa zichukuliwe” kama matukio ya utovu wa nidhamu katika kandanda hayataangamizwa.

Ripoti iliyotolewa na Fare network, shirika la kupambana na ubaguzi katika kandanda, na Kituo cha SOVA chenye makao yake mjini Moscow, inaonyesha kuwa Urusi imesakamwa na utamaduni wa mashabiki kuwa na tabia za kibaguzi na hisia kali.

Blatter alizungumza mwezi Julai mwaka jana na Rais wa Urusi Vladmir Putin akimtaka alipatie kipau mbele suala la kupambana na matukio ya kibaguzi, lakini visa vya uovu huo vinaendelea kutoa picha mbaya kwa nchi hiyo mwenyeji wa Kombe la Dunia 2018, pamoja na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com