Blair aendelea na ziara ya mashariki ya kati | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Blair aendelea na ziara ya mashariki ya kati

Tony Blair afanya ziara ya kwanza katika mashariki ya kati kama mjumbe wa pande nne zinazoshughulikia mgogoro wa eneo hilo.

Tony Blair na rais Shimon Peres wa Israel

Tony Blair na rais Shimon Peres wa Israel

Mjumbe wa pande nne zinazoshughulikia mgogoro wa mashariki ya kati bwana Tony Blair leo amekutana na rais Shimon Peres wa Israel mjini Jerusalem.Bwana Blair pia amefanya mazungumzo na rais Mahmoud Abbas wa Palestina.

Akizungumza katika ziara yake ya kwanza kama mjumbe wa mashariki ya kati ,bwana Tony Blair amewataka viongozi wa Israel na Palestina watumie fursa iliyojitokeza sasa katika eneo la mashariki ya kati.

Bwana Blair anaeziwakilisha , Marekani, Umoja wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa katika mchakato wa kuleta amani mashariki ya kati amesema kuwa ameweza kuona hisia mpya za uwezekano na hisia za utayarifu wa kusonga mbele katika mazungumzo.Hatahivyo ameeleza kuwa iwapo uwezekano uliopo utatumiwa, itategemea na juhudi zitakazofanyika.

Baada ya mazungumzo yake na rais Shimon Peres mjini Jerusalem , bwana Blair alisisitiza umuhimu wa kufanya juhudi zaidi ili kutatua mgogoro wa mashariki ya kati.

Bwana Blair pia amekutana na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas katika mji wa Ramallah.

Rais Abbas alieleza kuwa alipata fursa ya kuzungumza juu ya hali ya sasa katika mashariki ya kati na mchango unaotolewa na pande nne zinazoshughulikia mgogoro wa eneo hilo.

Hatahivyo chama chaa Hamas kimesema kuwa juhudi za bwana Blari hazitafanikiwa ikiwa atawapuuza wawakilshi wa chama hicho kilichoshinda uchaguzi wa b unge mwezi januari mwaka jana.Lakini msemaji wa bwana Blair amesema hapatakuwa mazungumzo yoyote baina mjumhe huyo an wawakilishi w a Hamas.

AM.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com