BLACKSBURG : Jopo kuchunguza mauaji ya Virginia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BLACKSBURG : Jopo kuchunguza mauaji ya Virginia

Gavana wa jimbo la Virginia nchini Marekani ameteuwa jopo la kujitegemea kuchunguza shambulio la risasi la Jumatatu katika Chuo Kikuu cha Virginia.

Tim Kaine ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba tume hiyo itachunguza jinsi mauaji hayo yalivyotokea na namna serikali ilivyochukuwa hatua.

Awali polisi ya Virginia ilielezea kutoridhishwa kwao kutokana na kituo cha televisheni cha NBC na vyombo vyengine vya habari kuonyesha ukanda wa video uliotumwa na mwanafunzi wa Korea Kusini Cho Seung- Hui mwenye umri wa miaka 23 ambaye amewauwa watu 32 pamoja na kujiuwa yeye mwenyewe katika chuo kikuu hicho cha Virginia.

Mkuu wa Polisi Steve Flaherty pia ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba kifurushi cha video na picha zilizotumwa na muuaji huyo hazikusadia sana katika uchunguzi wao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com