1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK:Serikali na upinzani zafikia makubaliano juu ya katiba

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv2

Serikali na maafisa wa upinzani nchini Kyrgyzstan wamefikia makubaliano na rais Kurmanbek Bakiyev juu ya katiba ambayo huenda yakasaidia kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.

Ghasia zilizuka jana kati ya wafuasi wa serikali na upinzani katika mji mkuu Bishkek.

maelfu ya wafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana mjini humo kudai katiba mpya itakayopunguza madaraka ya rais jambo ambalo limezusha mzozo wa kisiasa nchini humo .

Kiasa cha watu 35 walijeruhiwa katika mapambano ya hapo jana ambapo polisi walitumia gesi za kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa pande hizo mbili.