Bishkek. Kyrgystan yatolewa mwito wa kufanya mageuzi ya kidemokrasia. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bishkek. Kyrgystan yatolewa mwito wa kufanya mageuzi ya kidemokrasia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa wito kwa viongozi nchini Kyrgystan kutatua mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo kwa njia ya amani.

Katika mkutano mjini Bishkek mapema leo , Steinmeier amemwambia rais Kurmanbek Bakiyev na maafisa wengine wa ngazi ya juu kuwa Kyrgystan inapaswa kuendelea katika njia yake kuelekea mageuzi ya kidemokrasia ili kuweka heshima iliyojipatia miongoni mwa mataifa ya Ulaya.

Wakati huo huo , waandamanaji wameendelea kufanya maandamano kwa muda wa siku ya tatu mfululizo wakimtaka rais rais Bakiyev ajiuzulu kwa kutofanya juhudi za kutosha kupambana na ulaji rushwa.

Viongozi wa upinzani wamesema kuwa watasusia kikao cha Jumatatu cha bunge kitakachojadili mageuzi ya katiba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com