1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK: Katiba mpya yatiwa saini na rais wa Kyrgyzstan

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuU

Rais Kurmanbek Bakiyev wa Kyrgyzstan,ametia saini katiba mpya inayopunguza mamlaka yake.Katiba mpya iliyoidhinishwa na bunge siku ya Jumatano, italipa bunge mamlaka ya kumchagua waziri mkuu, ambae hapo zamani alikuwa akiteuliwa na rais wa nchi.Katiba hiyo mpya inatazamiwa kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.Siku ya Jumanne ghasia zilizuka baada ya wafuasi wa rais Bakiyev kupambana na wafuasi wa upinzani katika mji mkuu Bishkek.