1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Biden na Putin kukutana mjini Geneva

16 Juni 2021

Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wanakutana leo Jumatano mjini Geneva kwa mazungumzo ya kwanza ambayo hayabebi matumaini makubwa ya kumaliza tofauti zilizopo kati ya Washington na Moscow.

https://p.dw.com/p/3v0De
Flaggen von Russland und den USA
Picha: Sascha Steinach/dpa/picture alliance

Wakiwa njiani kuelekea mjini Geneva, afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Marekani amesema hawana matarajio ya kupatikana mafanikio makubwa kwenye mkutano huo kati ya Biden na Putin utakaofanyika kwa muda saa tano.

Matamshi sawa na hayo yametolewa pia na mshauri wa sera za kigeni wa rais Putin, Yuri Ushakov ambaye amesema hakuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano yoyote kwenye mkutano huo.

Hata hivyo pande zote mbili zimesema mazungumzo baina ya viongozi hao wawili ni muhimu kuelekea mahusiano thabiti na yanayotabirika kati ya Washington na Moscow ambazo zimeshuhudia mahusiano yakitetereka hadi kiwango cha chini kabisa miaka ya karibuni.