Bibi Bhutto kizuizini | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Bibi Bhutto kizuizini

Waziri mkuu wa zamaniwa Pakistan benazir bhutto amemtaka leo jamadari Musharraf kun'gatuka.Serikali ya pakistan ilimuweka jana bibi Bhutto kwa mara nyengine kizuizini nbyumbani.

Benazir Bhutto kizuizini nyumbani.

Benazir Bhutto kizuizini nyumbani.

Kiongozi wa upinzani nchini Pakistan,bibi Benazir Bhutto, amemtaka hii leo mtawala wa kijeshi wa Pakistan,jamadari Perverz Musharraf kujiuzulu.

Bibi Bhutto kwa mara nyengine tena amewekwa kizuizini nyumbani mwake.

Mkuu wa polisi wa Lahore,Aftab Cheema, amearifu kwamba waziri mkuu huyo wa zamani atabakia kizuizini kwa wiki moja.

“wakati umewadia kwa jamadari musharraf kun’gatuka madarakani.Analazimika kuoachamatangu madaraka ya urais hata ya mkuu wa majeshi.”

Bibi Bhutto,amewaambia leo waandishi habari kwa njia ya simu kutoka nyumba yake mjini Lahore.Huko amewekwa kizuizini tangu jana ili kumzuwia asiongoze maandamano marefu dhidi ya serikali ya jamadari Musharraf.

Bhutto akasema na ninamnukulu tena,

“Musaharraf haelewi kabisa jinsi hali ya kisiasa ilivyo mbaya wakati huu nchini .Amekuwa kipingamizi katika njia ya kwendea demokrasi na kwahivyo apaswa kutokomea.Ikiwa demokrasia haitarejeshwa ,hatima ya Pakistan iko hatarini.” Hii ni mara ya kwanza kwa Benazir Bhutto kumtaka jamadari Musharraf kuacha madaraka ya urais kwavile amkuwa akijadiliana nae kwa miezi kadhaa sasa kugawana nae madaraka.

Uhusiano wao lakini sasa umepooza kwavile jamadari Musharraf alienyakua madaraka 1999,ametangaza hali ya hatari hapo novemba 3 katika hatua ambayo wengi waamini imelengwa kumzuwia hakimu wa hgadhi ya juu asipitishe hukumu dhidi ya kuchaguliwa kwake tena.

Benazir Bhutto ameondosha sasa uwezekano wowote wa kufanya kazi pamoja na jamadari Musharraf alieahidi kufanya uchaguzi mkuu kama ilivyopangwa mnamo wiki ya kwanza ya Januari,mwakani.

“Sitapendelea hata kutumika kama waziri mkuu chini yake.” Alisema Benazir Bhutto.

Nae mkuu wa kikosai cha Polisi mjini Lahore,Aftab

Cheema alisema,

“Serikali imepiga marufuku maandamano mjini Lahore.Kwavile kuna kitisho kwa usalama,mikutano ya hadhara na maandamano ni marufuku.Tutajaribu kuzuwia matumizi ya nguvu.Sheria itachukua mkondo wake.”

Alisema Aftab Cheema,mkuu wa polisi mjini Lahore.

Katika duru za waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto inavuma kwamba chama chake kinapanga kusonga mbele na maandamano yake ya masafa ya kiasi cha km 300 kutoka Lahore hadi Islamabad.

“Mtu akijaribu kutuzuwia,mkoa mzima wa Punjab utageuka medani ya vita.” Alitishia hivyo msemaji wa Benazir Bhutto.

Nae Latif Khosa, mbunge wa chama Benazir Bhutto akaongeza:

“Mpango wa kuandamana upo pale pale.Tumewataka wafuzasi wetu kujiunga na maandamano hayo.

Kila mahala watakusanyika watu na kujaribu kuvuka vizuwizi vya polisi.Polisi imewatia nguvuni maalfu ya wafuasi wa chama chetu jana usiku.Wamesaka magari na kuyatia nguvuni.Lahore nzima inajikuta katika hali ya kuzingirwa.Na hii ndio sura ya demokrasia nchini Pakistan.”

Upinzani nchini Pakistan unadai kufutwa hali ya hatari,kurejeshwa kutumika kwa katiba pamoja na kuachwa huru kwa wote waliokamatwa.

Isitoshe, mbinyo dhidi ya jamadari Musharraf unazidi ulimwenguni.Serikali ya Marekani inamtaka jamadari Musharraf kama vile Jumuiya ya madola-C-wealth- avue mavazi yake ya kijeshi na aheshimu haki za kidemokrasia kama vile zile za kuandamana .Mawaziri wa nje wa C-wealth wamempa jamadari Musharraf muda hadi Novemba 22 kuitikia madai hayo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com