Bhutto arejea Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Bhutto arejea Pakistan

Benazir Bhutto aahidi kurejesha demokrasia

default

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhuto amerejea nyumbani machozi yakimdondoka,baada ya miaka minane uhamishoni.Amelahikiwa na umati wa watu laki mbili na nusu mjini Karachi,mji uliogeuzwa ngome kufuatia uvumi huenda waafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam wakajiripua.

Bibi Benazir Bhutto alisita kidogo kabla ya kuteremsha mguu katika ardhi ya nchi yake katika uwanja wa ndege wa Karachi.

Wafuasi wake wamemiminika kutoka kila pembe ya Pakistan.Kuna walioutwanga mguu,kuna waliokuja kwa treni,mabasi,magari na wengine kwa mapiki piki.Baadhi yao wamepitisha siku 12 njiani hadi Karachi.Polisi wanasema umati wa watu laki mbili na nusu umemlahiki Benazir Bhutto katika uwanja wa ndege.Lakini viongozi wa chama chake cha Pakistan Peoples Party wanazungumzia juu ya watu zaidi ya milioni moja waliokuja kumpokea.

Akivalia mavazi asilia-panjab ya rangi ya kijani,suruwali na mtandio mweupe-rangi za bendera ya Pakistan,Benazir Bhutto alianza kutokwa na machozi na kulia akisema tunanukuu:

“Nimekua mtu mzima sasa,nimejifunza mengi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita,lakini tutaendelea daima kupambana na utawala wa kiimla.”Tunataka kuwatimua wafuasi wa itikadi kali na kujenga taifa bora la Pakistan.”Mwisho wa kumnukuu.

Amerejea Pakistan,nchi aliyoipa kisogo mwaka 1999, ili kuepuka mashtaka ya rushwa dhidi yake.

Benazir Bhutto,aliyewahi kua waziri mkuu mara mbili nchini Pakistan,mwaka 1988 hadi 1990 na baadae kati ya mwaka 1993 hadi 1999,ameahidi kurejesha demokrasia katika nchi hiyo minayoongozwa na jenerali Pervez Musharaf tangu maapinduzi ya kijeshi ya october 99.

Anapanga kukiongoza chama chake cha Pakistan People’s Party PPP katika uchaguzi wa bunge kati kati ya mwezi January mwakani.

Benazir Bhutto anasema:

´“Nnnajaribu kuwaleta pamoja wote wale waliowahi kuchangia kuiongoza Pakistan katika njia ya demokrasi.Ndio maana nimezungumza na jenerali Musharaf kuhusu kuipindi cha mpito kuelekea demokrasia.Nataraji huu ni mwanzo wa kumalizika enzi za kiimla na kuingia katika enzi za demokrasia,hata kama bado ni mapema kuashiria jambo hilo.“

Jiji la Karachi limegeuzwa ngome inayolindwa vikali na vikosi 20 elfu vya usalama.Baada ya kuwasili Benazir Bhutto alipanda ndani ya lori kubwa lililopambwa kwaajili yake na kuanza kulizunguka jiji hilo la wakaazi milioni 12.Sherehe zimepangwa kuendelea kwa muda wa saa 18 ambapo bibi Benazir Bhutto amepangiwa kuuzunguka mji wa Karachi kuanzia uwanja wa ndege hadi katika Quba la muasisi wa Pakistan Muhammad Ali Jinnah.

 • Tarehe 18.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C77h
 • Tarehe 18.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C77h

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com