Berlusconi ahukumiwa kifungo | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.03.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Berlusconi ahukumiwa kifungo

Mahakama moja nchini Italia imemhukumu waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Silvio Berlusconi kwenda jela mwaka mmoja kuhusiana na kuchapishwa katika gazeti moja linalomilikiwa na familia yake maelezo yaliyonaswa kwa siri.

Italy's former Prime Minister Silvio Berlusconi wipes his face on a television show in Rome in this February 20, 2013 file photo. An Italian court on March 7, 2013 sentenced Berlusconi to a one-year jail term for making public the taped contents of a confidential phone call in a case related to a 2005 banking scandal. REUTERS/Remo Casilli/Files (ITALY - Tags: POLITICS MEDIA CRIME LAW)

Waziri mkuu wa zamani wa Silvio Berlusconi

Kwa mujibu wa sheria za mfumo wa kisheria nchini Italia ina maana kuwa kiongozi huyo wa zamani tajiri mwenye umri wa miaka 76 , hatahitajika kwenda jela hadi pale hatua za rufaa zitakapofikia mwisho, na mahakama ya juu huenda bado ikabadilisha uamuzi huo.

Hatua hii imekuja katikati ya mkwamo mkubwa wa kisiasa unaojitokeza kutokana na kutofikisha mwisho hatua za uchaguzi wiki iliyopita , uchaguzi ambao haukutoa kwa chama chochote uwezo wa kuunda serikali kwa wingi ilionao , licha ya kuwa muungano wa Berlusconi wa nadharia za mrengo wa wastani kulia ulijitokeza kuwa ni nguvu ya pili katika bunge.

talian Premier Silvio Berlusconi shows a Friday March 6, 1953 copy of the then Italian Communist Party official newspaper L'Unita, bearing banner headlines reading in Italian 28.02.2013

Silvio Berlusconi

Akabiliwa na kesi nyingi

Berlusconi anakabiliwa na mlolongo wa kesi , huku kesi tofauti kuhusiana na madai ya kukiuka kulipa kodi na kumlipa msichana mwenye umri mdogo fedha kwa madhumuni ya kufanya nae ngono ikikaribia kufika mwisho mwezi huu.

Amekana kuwa hana hatia ya kufanya kitu chochote kinyume na sheria katika kesi hiyo na hukumu hii imekosolewa na wakili wake Piero Longo, ambaye mara nyingi amemshutumu jaji Milan kuhusiana na keshi kadha zinazomkabili Berlusconi katika miaka kadha.

"Sikushangazwa kutokana na kwamba ni Milan na inamhusu Berlusconi," amewaambia waandishi habari baada ya hukumu hiyo.

"Lakini nina wasi wasi na kushutushwa kwasababu nina hakika kabisa kuwa madai dhidi ya Berlusconi yalikuwa dhaifu na yenye utata na hata kuwa hayakustahili kuwapo kabisa".

Former PM Berlusconi smiles as he casts his vote at the polling station in Milan Former Prime Minister Silvio Berlusconi smiles as he casts his vote at the polling station in Milan, February 24, 2013. Italians began voting on Sunday in one of the most closely watched elections in years, with markets nervous about whether it can produce a strong government to pull Italy out of recession and help resolve the euro zone debt crisis. REUTERS/Stefano Rellandini (ITALY - Tags: POLITICS ELECTIONS)

Berlusconi akipiga kura wakati wa uchaguzi wa bunge

Kaka yake Berlusconi Paolo , mkuu wa gazeti linalomilikiwa na familia hiyo la Giornale Daily , amehukumiwa kwenda jela miaka miwili na miezi mitatu kuhusiana na kesi hiyo hiyo, ambayo imehusika zaidi na maelezo yaliyonaswa kwa siri , yanayohusu ununuzi wa benki , maelezo ambayo yalichapishwa katika gazeti hilo.

Fidia

Mahakama pia imempatia kiasi cha euro 80,000 kama fidia Piero Fassino , ambaye alikuwa mkuu wa chama cha mrengo wa wastani kushoto katika wakati wa tukio hilo na ambaye matamshi yake yalinaswa katika ukanda na kuchapishwa katika gazeti hilo.

Fassino amesisitiza kuwa Giornale, ambalo ni gazeti la mrengo wa kulia lilichapisha maelezo hayo muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2006 ili kujenga mazingira kuwa Fassino amechukua hatua ambazo zinaweka mbinyo katika ununuzi wa benki ya Banca Nazionale del Lavono kwa kampuni ya bima ya Inipol mwaka 2005.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Yusuf, Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com