BERLIN.Waziri wa mambo ya nje ziarani ulaya ya mashariki | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN.Waziri wa mambo ya nje ziarani ulaya ya mashariki

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier amefanya mazungumzo mjini Moskow Urusi katika ziara yake ya Ulaya Mashariki.

Ujerumani ikiwa ndio inashikilia uenyekiti wa umoja wa ulaya inapanga pia kujadili swala la mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na hali ya baadae ya eneo la Serbia-Kosovo katika mkutano na maafisa wa Urusi.

Umoja wa Ulaya unaunga mkono mpango wa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Marti Ahtasaari unaopendekeza uhuru wa kadiri wa Kosovo.

Urusi inadai kuwa makubaliano ya aina yoyote ile lazima yakubaliwe na Serbia.

Utawala wa Serbia unapinga uhuru wa Kosovo ambao raia wengi katika eneo hilo wana asili ya Kialbania.

Katika ziara yake waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier ameandamana na mratibu wa sera za mambo ya nje wa umoja wa ulaya Javier Solana na kamishna wa uhusiano wa nje wa umoja wa ulaya Benita Ferrero- Waldner.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com