1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Uturuki yatakiwa kuondosha vikwazo vyake kwa Cyprus.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCva

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Uturuki lazima ichukue hatua katika mzozo wake na Umoja wa Ulaya juu ya kuitambua na kufanya biashara huru na Cyprus ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Ujerumani inaitaka Uturuki kuiondolea vikwazo vya kibiashara Cyprus lakini Uturuki inataka vikwazo vilivyowekwa na shirika la kibiashara duniani dhidi ya Cyprus kaskazini inayodhibitiwa na Uturuki viondolewe kwanza.

Uturuki imekataa kuitambua serikali ya Cyprus ya Ugiriki ambayo kimataifa inawakilisha kisiwa hicho katika umoja wa Ulaya.

Baada ya kikao cha dharura jana mjini Berlin kuzungumzia zamu ya Ujerumani kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya ifikapo Januari mosi mwakani, hasa kufuatia mzozo wa Cyprus, Kansela Angela Merkel amesema.

”Tutajadiliana kwa busara. Hatutaki malumbano ya kisiasa hiyo lakini inamaanisha pande zote na hasa Uturuki ziwajibike”.