BERLIN:Ujerumani yakataa kutimiza madai ya watekaji nyara | Habari za Ulimwengu | DW | 12.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Ujerumani yakataa kutimiza madai ya watekaji nyara

Nchi ya Ujerumani inashikilia kuwa haitatimiza madai ya watekaji nyara wanaowazuilia raia wake wawili nchini Iraq.Muda wa mwisho wa kuwaachia mateka hao unakwisha usiku wa leo mwendo wa saa sita.

Kulingana na Naibu waziri wa mashauri ya kigeni Gernot Erler kundi la kushughulikia masuala ya dharura linafanya kila liwezalo kluahkikisha kuwa mustakabal wa mateka hao ni salama.

Hannelore Kadhim na mwanawe Sinana aliye na umri wa miaka 20 walitekwa walipokuwa nyumbani kwao mjini Baghdad mwanzoni mwa mwezi wa pili mwaka huu na kundi lisilo na umaarufu linalojulikana kama Arrows of Righteousness.

Ukanda wa video unaonyesha mateka hao wakiomba kufanyiwa hisani ulisambazwa katika mtandao na watekaji nyara hao wanaotoa wito wa kuondolewa kwa majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan.

Kundi hilo liliwaeleza mateka hao Hannelore Kadhim aliyeolewa na raia wa Iraq kuwa afisa wa ngazi za juu katika ubalozi wa Austria nchini humo…nchi ambayo kulingana nao si rafiki wa dini ya Kiislamu.Aidha mwanawe…Sinana Kadhim ni mfanyikazi wa Wizara ya mambo ya nje ya Iraq.

Ujerumani ilipeleka yapata majeshi alfu 3 nchini Afghanistan kuhusika na shughuli za ukarabati katika maeneo ya kaskazini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com