1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani yakataa kuinga mkono Ufaransa

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOj

Ujerumani imejiweka mbali na kauli iliyotolewa na Waziri wa Mmabo ya Nje wa Ufaransa Bernard Kouchner juu ya uwezekano wa kushambuliwa kijeshi Iran.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani akizungumza mjini Berlin amesema kuwa Ujerumani inajaribu kufikia muafaka wa mzozo huo wa mtambo wa nuklia wa Iran.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomic la Kimataifa Mohamed El Baradei ameelezea imani yake ya kupatikana suluhu la mzozo huo kwa njia za kidiplomasia.

Wakati huo huo Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi yake hailipi uzito onyo hilo la waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa.