1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Uchumi kustawi kwa asilimia 2.2 katika mwaka ujao

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7En

Wataalam wa uchumi wametoa mwito kwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel juu ya kusonga mbele na mageuzi kwa mwendo wa kasi zaidi.

Wataalamu hao wametoa mwito huo katika ripoti juu ya uchumi wa Ujerumani unaotabiriwa kuwa ustawi utafikia asilimia 2.2 katika mwaka ujao badala ya asilimia 2.4.

Hata hivyo wamesema ustawi katika mwaka huu utafikia asilimia 2.6 kadhalika wametabiri kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kwamba Ujerumani itakuwa na bajeti itakayofikia ziada.