BERLIN:Rais Köhler ahimiza shirka la IMF liachwe huru kutenda kazi zake | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Rais Köhler ahimiza shirka la IMF liachwe huru kutenda kazi zake

Rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Köhler ametoa mwito kwamba shirika la fedha duniani IMF lipewe uwezo juu ya kushughulikia masoko ya fedha duniani bila pingamizi kutoka upande wowote.

Katika hotuba yake ya mwaka mjini Berlin Rais Köhler aliyewahi kuliongoza shirika la fedha duniani la IMF amesema shirika hilo linapaswa kuachwa huru kufanya kazi zake kwa manufaa na utulivu katika mpango wa fedha wa kimataifa.

Hotuba ya mwaka ya rais Horst Köhler ilituwama katika faida ya utandawazi hasa kuelekea nchi masikini.

Rais wa Shairikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler amesisitiza kwamba njia bora ya kuzisaidia nchi masikini ni kuzipa nafasi katika masoko ya nchi zilizo endelea kiviwanda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com