BERLIN:Kansela Merkel aahidi kufufua mchakato wa katiba ya Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 12.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Kansela Merkel aahidi kufufua mchakato wa katiba ya Umoja wa Ulaya

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuwa serikali yake inakusudia kufanya juhudi ili katiba ya Umoja wa Ulaya ipitishwe.

Ujerumani itakuwa rais wa Umoja wa Ulaya kwa muda wa miezi sita kuanzia mwezi wa januari mwaka ujao.

Bibi Merkel amesema, katika kipindi hicho serikali yake itatekeleza mpango maalumu, ili katiba ya Umoja huo ipitishwe.

Katiba hiyo haikuweza kuidhinishwa na nchi za Ulaya baada ya idadi kubwa ya wananchi wa Ufaransa na Uholanzi kuikataa katika kura za maoni zilizofanyika mwaka jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com