BERLIN: Waziri asema kadhia ya Murat Kurnaz ilishughulikiwa kwa msingi wa kiusalama. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Waziri asema kadhia ya Murat Kurnaz ilishughulikiwa kwa msingi wa kiusalama.

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Otto Schily amemtetea Waziri wa Mambo ya nje, Frank-Walter Steinmeier kwa madai dhidi yake kwamba alikataa raia wa Ujerumani mwenye asili ya Kituruki kuachiwa huru kutoka gereza la Marekani la Guantanamo.

Murat Kurnaz hatimaye aliachiwa huru mwezi Agosti mwaka uliopita, miaka mitano baada ya kukamatwa nchini Pakistan kwa tuhuma za ugaidi.

Murat Kurnaz hakufunguliwa mashtaka yoyote.

Otto Schily alisema kadhia ya Murat Kurnaz ilihusu zaidi maswala ya usalama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com