BERLIN: Wanajeshi wakiri kudhalilisha wafu | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Wanajeshi wakiri kudhalilisha wafu

Generali wa Ujerumani amesema wanajeshi watatu wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr wamekiri kuhusika na udhalilishaji wa wafu nchini Afghanistan na kuelezea majuto yao juu ya vitendo vyao hivyo.

Awali Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani ilisema wapepelezi wamekuwa wakiwahoji watuhumiwa 20 kuhusiana na picha za wanajeshi wakiwa na bufuru la binaadamu ambazo zilichapishwa mara ya kwanza na gazeti mashuhuri la Bild nchini Ujerumani. Wizara hiyo ya ulinzi imekanusha repoti kwamba maafisa wa jeshi la Ujerumani nchini Afghanistan walikuwa wakijuwa kwa muda mrefu juu ya kuwepo kwa picha hizo kabla ya habari hizo kutangazwa.

Wanajeshi wawili walisimamishwa kazi wiki iliopita kwa kuhusika na tukio hilo.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekielezea kitendo hicho kuwa hakina kisingizio na kusema kwamba wahusika wataadhibiwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com