BERLIN: Wajerumani washerehekea mwaka mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Wajerumani washerehekea mwaka mpya

Wajerumani zaidi ya milioni moja walikusanyika kwenye barabara za mji mkuu Berlin kwa sherehe za mwaka mpya. Mamia ya maelfu walikusanyika katika lango maarufu la Bandenburg kama ilivyokuwa wakati wa michuano ya kuwania kombe la kandakanda la dunia mwaka uliopita.

Ilipofika saa sita usiku wa kuamkia leo, Ujerumani ilichukua urais wa Umoja wa Ulaya ambao sasa umepata wanachama wawili wapya, Bulgaria na Romania. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, akiwa mjini Bucharest nchini Romania aliwaambia maofisa wa Romania kwamba wamesafiri safari ndefu na ngumu na kuwakaribisha katika Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo, Slovenia itaanza kutumia sarafu ya euro hivyo kuwa taifa la kwanza lililokuwa hapo zamani la kikomunisti, kutumia sarafu hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com