1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Vikosi vya Kijerumani vyakamilisha ujumbe wake Kongo

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCo6

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz-Josef Jung amesifu ujumbe wa vikosi vya Kijerumani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wakati huo huo msemaji wa majeshi ya Ujerumani mjini Kinshasa amesema vikosi vya Umoja wa Ulaya vilivyopelekwa Kongo kusimamia usalama vimechangia kuleta utulivu nchini humo.Rasmi,ujumbe huo unamalizika leo hii.Inatazamiwa kuwa hadi Desemba 22 wanajeshi wote wa Kijerumani watakuwa wamerejea nyumbani.Vikosi hivyo vilisaidia kulinda amani wakati wa kufanywa uchaguzi huru wa mwanzo baada ya zaidi ya miongo minne nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.