1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Vikosi vya Kijerumani havitopelekwa kusini mwa Afghanistan

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsy

Serikali ya Ujerumani imeamua kutotuma vikosi vyake katika maeneo ya mapigano makali kusini mwa Afghanistan.Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema,majeshi ya Ujerumani yamechukua dhamana kaskazini mwa nchi na yatabakia huko huko.Shirika la NATO lilisema majeshi ya shirika hilo yasiwekewe mipaka.Wakati huo huo Ujerumani imesema kuwa haitopeleka vikosi vyake kupigana nchini Irak na vile vile itakamilisha ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tarehe 30 mwezi huu kama ilivyopangwa.Hayo yalitangazwa na waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung na msemaji wa wizara ya ulinzi Thomas Raabe katika mikutano mbali mbali na waandishi wa habari kueleza mustakabali wa wanajeshi 9,000 wanaoshiriki katika operesheni katika nchi za ngámbo.Raabe akaongezea kuwa Ujerumani itafikiria kurefusha mafunzo yanayotolewa kwa polisi na wanajeshi wa Kiiraki.Wakati huo huo waziri Jung alisema kuwa operesheni ya Kongo kusimamia usalama na amani wakati wa uchaguzi wa rais nchini humo imefanikiwa.