1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Umoja wa Ulaya una wasiwasi juu ya Iran

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAm

Ujerumani ambayo ni rais wa Umoja wa Ulaya inasema ina wasiwasi juu ya tangazo la Iran kwamba iko tayari kuanza kurutubisha uranium kwa kiwango kikubwa.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mashauri ya kigeni mjini Berlin imesisitiza mwito wa Umoja wa Ulaya kuitaka Iran itii masharti ya jumuiya ya kimatiafa na irejee kwenye meza ya mazungumzo.

Wakati wa sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Iran ilipofaulu kurutubisha uranium, rais wa Iran, Mahmoud Ahamadinejad, alisema nchi yake iko tayari kuanza kurutubisha madini ya uranium kwa kiwango kikubwa.

Wakati huo huo, kiongozi wa shirika la nishati ya nyuklia la Iran amesema wanalenga kuweka mashinepewa elfu 50 katika kiwanda cha Natanz.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ameitaja hatua ya Iran kuwa ukaidi dhidi ya jumuiya ya kimatiafa.