BERLIN: Ukeketaji wa wanawake na wasichana upigwe marufuku kisheria | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Ukeketaji wa wanawake na wasichana upigwe marufuku kisheria

Kwa kuadhimishwa siku ya kimataifa dhidi ya ukeketaji,mjumbe wa serikali ya Ujerumani anaehusika na masuala ya haki za binadamu na misaada ya kiutu katika wizara ya nje,Günter Nooke ametoa wito wa kupiga marufuku kisheria tabia hiyo.Amesema,ingawa maendeleo yamepatikana katika jumuiya ya kimataifa kulaani kitendo hicho,sasa nchi zinazohusika zinapaswa kuchukua hatua rasmi za kisheria.Akaongezea kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 100 wameathirika kiafya sehemu mbali mbali duniani kwa sababu ya ukeketaji.Nooke hivi sasa,anazizuru Togo,Liberia na Sierra Leone kwa majadiliano yanayohusika na haki za binadamu na hali ya kiutu katika nchi hizo za Afrika ya Magharibi,kwa hivyo suala la ukeketaji pia ni mada mojawapo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com