1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani yakubali kiwago cha utowaji wa gesi CO2

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTq

Gazeti la Tageszeitung limesema Ujerumani imekubali kiwango kilichowekwa na kamati kuu ya Umoja wa Ulaya juu ya utowaji wake wa carbon dioxide gesi ambayo inalaumiwa kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Utowaji wa gesi hiyo kwa Ujerumani utakuwa kwenye kiwango cha tani 453 kwa mwaka ikiwa ni pungufu kwa asilimia mbili ya kiwango ilichokuwa imetaka Ujerumani.Kwa mujibu wa gazeti hilo la Ujerumani waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel ambaye yuko ziarani nchini Kenya amesema Ujerumani imekubali kufikia muafaka huo ili kuonyesha kwamba inaunga mkono mfumo wa Umoja wa Ulaya wa kubadilishana hati za utowaji wa gesi zinazoathiri mazingira.

Shirikisho la Viwanda nchini Ujerumani limesema kiwango hicho kipya kitayagharimu mno makampuni.