BERLIN: Uchumi wa Ujerumani unatarajiwa kukua kwa kiwango kikubwa mwaka huu | Habari za Ulimwengu | DW | 07.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Uchumi wa Ujerumani unatarajiwa kukua kwa kiwango kikubwa mwaka huu

Serikali ya Ujerumani inahakika kukua kwa uchumi wake kutaimarika zaidi mwaka huu kama ilivyotarajiwa hapo awali.

Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Michael Glos, ameliambia gazeti la Bild am Sonntag kwamba kiwango cha asilimia 1,7 cha ukuaji wa uchumi kilichowekwa hapo awali, huenda kikaongezwa.

Waziri Glos amesema kunawiri kwa uchumi huenda kukalinufaisha soko la ajira huku idadi ya watu wasio na ajira ikishuka chini ya idadi ya watu milioni 3.5 wakati wa msimu wa machipuko.

Watu wasio na ajira nchini Ujerumani ni zaidi ya milioni nne.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com