1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Stoiber yuko njia moja.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaF

Nchini Ujerumani , chama ndugu ya chama cha kansela Angela Merkel kinahangaika kuhusiana na hatima ya kiongozi wake, waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Edmund Stoiber.

Katika siku ya kwanza ya mkutano wa siku mbili wa chama cha CSU, Stoiber ameonyesha ishara kwa mara ya kwanza kuwa hahitaji kuwa kugombea nafasi ya uongozi wa chama hicho kwa mara nyingine mwaka ujao.

Uungwaji mkono kwa Stoiber , ambaye ameliongoza jimbo la Bavaria kwa muda wa miaka 14, umeshuka katika chama cha CSU kufuatia madai ya kuwa alifanya ujasusi dhidi ya mahasimu wake katika chama hicho. Mzozo huo unaweza kusababisha matatizo kwa chama cha Merkel cha Christian Democratic, ambacho kina makubaliano na chama cha CSU tangu mwaka 1949.