1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Steinmeir kutowa ushahidi

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjN

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir anatazamiwa kufika mbele ya kamati ya bunge yenye kuchunguza ushirikiano kati ya serikali ya Ujerumani na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kwa kile Marekani inachokiita vita vya ugaidi.

Steinmeir ambaye alikuwa waziri wa nchi katika ofisi ya Kansela anatazamiwa kuieleza kamati hiyo ni wakati gani serikali ya Ujerumani ilijuwa juu ya kutekwa nyara kwa Khaled el Masri raia wa Ujerumani mwenye nasaba ya Lebanon.Gazeti la Ujerumani la Berliner Zeitung limeripoti kwamba Steinmeir alipata habari juu ya kutekwa nyara kwa el Masri na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA mwezi wa Januari mwaka 2005 lakini hakuwaambia hayo maafisa wa kuendesha mashtaka ya uhalifu au kamati ya udhibiti bungeni.

El Masri alikamatwa nchini Macedonia mwishoni mwa 2003 na anasema alifungwa gerezani na CIA kwa miezi kadhaa nchini Afghanistan.