BERLIN : Raia wawili wa Ujerumani hawajulikani walipo Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 12.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Raia wawili wa Ujerumani hawajulikani walipo Iraq

Gazeti la Ujerumani linaripoti kwamba raia wawili wa Ujerumani wametekwa nyara nchini Iraq.

Gazeti la Berliner Morgenpost litolewalo kila siku limewakariri maafisa wa usalama wasiotajwa majina wakisema kwamba Wajerumani hao walikuwa wakikaa Baghdad na wamekuwa hawajulikani walipo kwa siku kadhaa sasa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amethibitisha mjini Brussels kwamba Wajerumani hao wamekuwa hawajulikani walipo kwa wiki moja sasa lakini haijulikani iwapo wametekwa nyara.

Mwaka jana Wajerumani wawili Rene Bräunlich na Thomas Nitzschke walitekwa nchini Iraq na kuachiliwa bila ya kudhuriwa miezi mitatu baadae.

Miezi kadhaa kabla mtaalamu wa machimbo ya kale Susanne Osthof alishikiliwa mateka kwa wiki kadhaa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com