BERLIN: Pelosi asifu jitahada za Merkel | Habari za Ulimwengu | DW | 29.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Pelosi asifu jitahada za Merkel

Spika wa Baraza la Wawakilishi katika Bunge la Marekani,Nancy Pelosi amemsifu Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa kile alichokiita, “uongozi wa kipekee” katika jitahada za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.Pelosi wa chama cha Demokrat,alitamka hayo baada ya kukutana na Merkel mjini Berlin.Vile vile aliahidi msaada wa Bunge la Marekani kutafuta makubaliano ya kitaifa kwa azma ya kupunguza ujoto duniani.Hayo ni kinyume kabisa na msimamo wa Rais George W.Bush, ambae miaka mitano iliyopita aliitoa Marekani kutoka Makubaliano ya Kyoto yanayotoa mwito kupunguza gesi zinazoathiri mazingira.Serikali ya Washington inashikilia kuwa malengo yote ya kupambana na ujoto duniani,yafutwe kwenye mswada wa taarifa itakayotolewa,mwishoni mwa mkutano wa kilele wa G-8.Msimamo huo ni tofauti kabisa na ule wa Bunge la Marekani ambalo hudhibitiwa na chama cha Demokrat.Mkutano wa madola tajiri yaliyoendelea kiviwanda duniani,G-8 utafanywa Heiligendamm nchini Ujerumani kuanzia tarehe 6 hadi 8 Juni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com