BERLIN: Mwito kwa Kansela Merkel kuishinikiza China | Habari za Ulimwengu | DW | 25.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Mwito kwa Kansela Merkel kuishinikiza China

Shirika la Amnesty International linalotetea haki za binadamu duniani,limetoa mwito kwa Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel kuishinikiza zaidi serikali ya China kuhusu sera za nchi hiyo juu ya haki za binadamu.

Amnesty International linasema,majadiliano yanayofanywa pamoja na Beijing hadi hivi sasa hayakuleta mafanikio makubwa.Katibu Mkuu wa Tawi la Amnesty International nchini Ujerumani,Bibi Barbara Lochbihler amesema,ana hofu kuwa kabla ya kufunguliwa kwa michezo ijayo ya Olimpiks mjini Beijing,serikali ya China huenda ikawashinikiza zaidi wapinzani na wahalifu,kwa kutoa adhabu zaidi za kifo,hiyo ikiwa ni kama njia ya kuwatisha wakosoaji wake.

Kansela Merkel anaanza ziara yake ya siku tano nchini China,siku ya Jumapili.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com