Berlin :Mpango wa waziri wa ndani Schäuble wakosolewa | Habari za Ulimwengu | DW | 16.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin :Mpango wa waziri wa ndani Schäuble wakosolewa

Waziri wa ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble anajaribu kupunguza mvutano katika serikali kuu ya mseto ya Shirikisho, uliosababishwa na mapendekezo yake ya karibuni kuhusu vita dhidi ya ugaidi. Mtaalamu wa maswala ya ndani wa chama cha Social Democrats SPD mshirika katika serikali kuu ya muungano Bw Dieter Wiefelspütz, aliliambia gazeti la kila siku Frankfurter Rundschau, kwamba Bw Schäuble amekua ni mzigo katika muungano huo.

Waziri huyo wa ndani kutoka chama cha Christian Democratic Union-CDU, amesema matamshi yake katika mahojiano juu ya kuwalenga na kuwauwa washukiwa wa ugaidi yalifahamika vibaya. Katika hatua isiyo ya kawaida, rais wa Ujerumani Horst Köhler alimkosoa hadharani Bw Schäuble mwishoni mwa juma lililopita, kwa mapendekezo yake juu ya kupambana na ugaidi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com