1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkuu wa chama cha kampuni za magari ajiuzulu

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKI

Mkuu wa Chama cha makampuni ya magari ya Ujerumani VDA amejiuzulu ghafla lakini amekanusha kwamba ni kwa sababu ya itikio baya la mjadala wa Ulaya juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Bernd Gottschalk amekuwa rais wa VDA tokea mwaka 1996.Jarida la habari la Spiegel limesema makampuni makuu ya magari nchini Ujerumani yalikuwa yakimshutumu Gottschalk kwa kudharau suala la mabadiliko ya hali ya hewa na kushindwa kuonyesha jitihada ambazo tayari zimechukuliwa na makampuni hayo kupunguza utowaji wa gesi za carbon di oxide.

Kundi jengine la kupiga debe ambayo ni klabu ya usafiri ya ekolojia VCD imeshutumu makampuni ya magari ya Ujerumani kwa kushindwa kutengeneza magari yenye kuzingatia utunzaji wa mazingira.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya hapo Ijumaa wamekubaliana kupunguza kwa asilimia 20 utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira na kuongeza mara tatu zaidi matumizi ya nishati zinazoweza kutumiwa upya za nguvu za upepo,jua na maji ifikapo mwaka 2020.