1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Migomo ya treni yafutwa kwa sasa

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBad

Chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni nchini Ujerumani GDL kimetangaza kwamba hakitofanya migomo zaidi wakati mazungumzo ya usuluhishi yakifanyika na shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn juu ya mzozo wa mishahara.

Mapema Deutsche Bahn na chama hicho cha wafanyakazi wamekubaliana juu ya kuwateuwa wasuluhishi kujaribu kusuluhisha mzozo huo ambao umepelekea kusita kwa muda kwa usafiri wa treni wa miji ya Berlin na Hamburg.

Migomo hiyo ambayo ilipangwa kuwa ya taifa zima kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 15 ingeliathiri watu milioni 5 kwa siku halikadhalia ingelizototesha uchumi wa Ujerumani ambao ndio wenye nguvu kubwa kabisa barani Ulaya.

Margaret Suckale mkuu wa idara ya wafanyakazi ya shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn anasema wanatumai kuanza mazungumzo kwa haraka ili kwamba kuwaepushia migomo zaidi wateja wao katika kipindi hiki cha mapumziko.

Chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni nchini Ujerumani GDL kinataka ongezeko la mishahara la asilimia 31 wakati shirika la reli la Deutsche Bahn limekubali kutowa asilimia 4.5.