BERLIN : Merkel kufufuwa amani Mashariki ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Merkel kufufuwa amani Mashariki ya Kati

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anapanga kufufuwa shughuli za kundi la pande nne kuleta amani Mashariki ya Kati ikiwa kama sehemu ya shughuli za uongozi wa nchi yake wakati itakaposhika hatamu ya Urais wa Umoja wa Ulaya hapo mwakani.

Katika ujumbe wake wa kila wiki kwa wapiga kura kwa njia ya mtandano Merkel amesema ni muhimu kwa kundi hilo la pande linalojumuisha Marekani,Urusi,Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kuanza kuangalia upya namna ya kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Mashariki ya Kati.

Kundi hilo liliianzisha mpango unaojulikana kama Ramani ya Amani hapo mwaka 2003 wenye kutaka kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina lakini hata hivyo juhudi hizo zimeshindwa kuzaa matunda.

Merkel anatarajiwa kukutana na Rais Housni Mubarak wa Misri mjini Berlin baadae leo hii kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert hapo Jumanne.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com