1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel aeleza sera ya Ujerumani kwa Ulaya

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjP

Wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakielekea mjini Brussels kwa mkutano wa viongozi wa siku mbili unaoanza leo hii Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametowa hotuba ya sera bungeni juu ya mipango ya Ujerumani wakati itakapochukuwa wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya hapo mwakani.

Ujerumani itachukuwa wadhifa huo kutoka Finland hapo mwezi wa Januari.Merkel ametumia hotuba yake hiyo kuuita kutanuka kwa Umoja wa Ulaya kwa kujumuisha mataifa ya ulaya ya mashariki kuwa ni mafanikio yasiostahili.Amesema mkutano huo wa viongozi utalenga juu ya namna umoja huo utakavyotanuka huko mbele.Pia amesema kwamba Umoja wa Ulaya unafuata mwelekeo thabiti lakini wa uangalifu kuhusiana na suala la Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuidhinisha uamuzi uliopitishwa na mawaziri wa mambo ya nje mapema wiki hii kusitisha kwa kiasi fulani mazungumzo ya uwanachama wa Uturuki kwa sababu ya kugoma kwake kufunguwa bandari zake zote kwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya Cyprus.

Mapema Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Manuel Barroso ameonya kwamba mazungumzo na Uturuki kujiunga na umoja huo yanaweza kuchukuwa miaka 15.