BERLIN: Makubaliano ya kufunga migodi ya makaa ya mawe | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Makubaliano ya kufunga migodi ya makaa ya mawe

Makubaliano ya mwisho yamepatikana kufunga migoodi ya makaa ya mawe nchini Ujerumani.Viwanda vya makaa ya mawe,kila mwaka hupokea kutoka serikalini,ruzuku ya zaidi ya Euro bilioni mbili. Wiki iliyopita ilikubaliwa kuwa migodi yote ya makaa ya mawe ifungwe,ifikapo 2008.Lakini serikali ya jimbo la North Rhine Westphalia, ambako sehemu kubwa ya migodi ya makaa hukutikana,ilipinga uamuzi huo na kusema kuwa gharama za ruzuku ni kubwa mno.Kuambatana na makubaliano mapya,serikali kuu ya Berlin kuanzia mwaka 2014,italipa sehemu ya gharama za jimbo la North Rhine Westphalia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com