BERLIN: Kansela wa Ujerumani amewasili Jordan | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Kansela wa Ujerumani amewasili Jordan

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akianza ziara yake ya siku tatu katika Mashariki ya Kati amepokewa nchini Jordan na Mfalme Abdallah wa Pili.Katika makao yake ya Aqaba,Mfalme Abdullah wa Pili alimuarifu Kansela Merkel juu ya matokeo ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Nchi za Kiarabu.Siku ya Alkhamisi,viongozi wa Kiarabu katika mkutano wa Riyadh nchini Saudi Arabia walikubaliana kufufua mpango wa amani wa mwaka 2002.Kuambatana na mradi huo wa amani,nchi za Kiarabu zitakuwa na uhusiano wa kawaida na Israel ikiwa itaondoka kutoka maeneo yaliyotekwa katika vita vya mwaka 1967 na itawaruhusu wakimbizi wa Kipalestina kurejea makwao.Kansela Merkel ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa urais unaozunguka kila miezi sita katika Umoja wa Ulaya,anataka kuimarisha utaratibu wa amani katika kanda ya Mashariki ya Kati.Ziara ya Merkel itampeleka pia nchini Israel,katika Maeneo ya Wapalestina na Lebanon.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com