BERLIN : Jung na utata wa makombora ya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Jung na utata wa makombora ya Marekani

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Josef Jung apunguza makali utata juu ya mipango ya Marekani ya kuweka makombora ya kujihami katika Ulaya ya mashariki.

Kufuatia mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates mjini Berlin Jung amesema anathamini ahadi ya Marekani kuendelea kuijulisha Ujerumani juu ya maendeleo ya mipango yao hiyo hatua kwa hatua.

Hata hivyo Urusi inaendelea kupinga vikali wazo la kuwa na makombora ya ulinzi ya Marekani katika nchi za Poland na Czeck. Gates amesisitiza pendekezo la Marekani la kushirikiana na Urusi data za makombora ya kutowa tahadhari pamoja na teknolojia ya mfumo huo wa makombora ya kujihami.

Serikali ya Marekani inasema makombora hayo ya kujihami yanahitajika kuilinda Marekani dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya makombora kutoka Mashariki ya Kati.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com