1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berin: Kansela Merkel wa Ujerumani azungumzia juu ya hatua ya Russia ya kuzuwia mafuta yanakuja Ujerumani kuoitia Belorussia.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHg

Kansela Angela Merkel amesema kusita hivi sasa kuja mafuta kutoka Russia hadi Ulaya Magharibi kumedhihirisha haja ya Ujerumani kuwa na njia nyingine za kupitia nishati inayoihitaji. Akizungumza katika televisheni ya Ujerumani, Kansela Merkel alisema serekali yake inahitaji kuzingatia matokeo ya mipango ya sasa ya kutaka kupunguza kutumia nishati ya kinyukliya.

+Tokeo hili, bila ya shaka, halijaleta athari kubwa sana katika sisi kupata nishati , lakini katika miaka ya karibuni yametokea kila wakati matatizo juu ya mafuta hayo yanakopitia hadi kuja hapa Ujerumani. Tunataka uhakika wa kisheria, tunataka uhakika katika mikataba tuliotia saini, na jambo hilo sasa linaonesha lazima lipanuliwe kuziingiza nchi ambazo mafuta hayo yanapitia. Mtu asifikirie tu kwamba mafuta hayo yanatokea kule yanakochimbwa na kuishia katika nchi yanakohitajiwa kutumiwa. Naamini sisi pia tufanye mazungumzo ya kina, na hali hii yote inahakikisha kwamba hapa Ujerumani tunahitaji kuwa na mchanganyikjo wa nishati za aina mbali mbali.+

Bibi Merkel alikuwa akizungumza masaa baada ya Russia kusitisha kupeleka mafuta kwa njia ya bomba kupitia kituo cha Druzhba kilioko Belorussia. Russia imesema Belorussia imkeuwa ikiyachukua mafuta yanayopitia katika ardhi yake kwa njia isiokuwa ya halali. Asili mia 20 ya mafuta yanayojia Ujerumani hupitia katika bomba la Druzhhba.