Benzema atimuliwa katika timu ya Ufaransa | Michezo | DW | 11.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Benzema atimuliwa katika timu ya Ufaransa

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema amesimamishwa kutoka timu ya taifa ya Ufaransa hadi uchunguzi wa madai yanayohusiana na kanda chafu ya ngono ukamilishwe

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 sasa huenda akakosa fursa ya kuchezea timu ya taifa katika michuano ya ubingwa wa Ulaya yaani UEFA Euro 2016 itakayoandaliwa nchini Ufaransa.

Benzema amesimamishwa kucheza na Shirikisho la Soka la Ufaransa - FFF. Benzema anachunguzwa kwa madai ya kujihusisha na ulaghai katika njama ya kutishia na kudai pesa kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena, madai ambayo anayakanusha.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com