1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki Kuu ya Ulaya yashusha kiwango cha riba

K.Zawadzky - (P.Martin)6 Machi 2009

Benki Kuu ya Ulaya imepunguza kiwango cha riba kwa asilimia 0.5 na hivyo kuangukia asilimia 1.5 tu. Hicho ni kiwango cha chini kabisa cha riba tangu sarafu ya Euro kuanza kutumiwa hiyo miaka kumi iliyopita.

https://p.dw.com/p/H6iR
Jean-Claude Trichet, Praesident der Europaeischen Zentralbank EZB, lauscht am Donnerstag, 2. Okt. 2008, im Anschluss an die EZB Ratssitzung in Frankfurt auf einer Pressekonferenz der Frage eines Journalisten. Die Europaeische Zentralbank hat die Zinsen fuer den Euroraum am Donnerstag, 2. Okt. 2008, wie erwartet unveraendert gelassen. Das teilte die EZB in Frankfurt am Main nach ihrer turnusmaessigen Sitzung mit. (AP Photo/Daniel Roland) --- Jean-Claude Trichet, President of the European Central Bank ECB listens to a journalist's question during a news conference in Frankfurt, central Germany, on Thursday, Oct. 2, 2008. The European Central Bank left its key interest rate unchanged at 4.25 percent Thursday as inflation fears outweighed the growing financial crisis that has crept through Europe. (AP Photo/Daniel Roland)
Jean-Claude Trichet,Rais wa Benki Kuu ya Ulaya.Picha: AP

Kupunguzwa kwa kiwango cha riba ni hatua itakayosaidia benki katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro na ilipaswa kuchukuliwa kwa sababu ya hali ya uchumi unaoendelea kudorora.Kwani habari mbaya zinazidi kumiminika katika masoko ya kiuchumi.Viwanda vinafuta maagizo yake, idadi ya makampuni yenye matatizo inaendelea kuongezeka na watu wasio na ajira wanongezeka. Kiwango cha riba kimeshushwa kwa sababu huu si wakati wa kupandisha bei.

Hatua iliyochukuliwa na Benki Kuu ya Ulaya ilikuwa ikipigiwa debe na Rais wa benki hiyo Jean-Claude Trichet tangu majuma kadha.Kwa hivyo benki wala hazikushtuka kwani hatua iliyochukuliwa na Benki Kuu ya Ulaya ni sahihi. Uchumi ulipoporomoka mwaka jana hasa kutokana na mzozo uliosababishwa na mikopo rahisi ya nyumba nchini Marekani,benki kuu kote duniani zilianza kupunguza viwango vya riba. Asilimia 1.5 ni kiwango cha chini kabisa kufikiwa katika kanda inayotumia Euro na huo si mwisho.Hali ya uchumi haijawahi kuwa mbaya hivi tangu miongo kadhaa.

Kwa mujibu wa uzoefu wa miaka iliyopita,kiwango cha riba kinaposhushwa,basi harakati za kibiashara huanza kuchangamka baada ya kama nusu mwaka.Kwani wafanya biashara hutumia fursa hiyo kuwekeza,kwa sababu ya mikopo rahisi na hata watu binafsi huchukua mikopo rahisi na matumizi yao huongezeka.Lakini safari hii,dawa hiyo haifanyi kazi hivyo kwani uchumi unaendelea kudorora na hakuna anaejua utaangukia wapi.Hata hivyo kiwango cha riba kilichopunguzwa kimezuia madhara makubwa zaidi.Kwa hivyo itakuwa busara kwa Benki Kuu ya Ulaya kuongojea hadi majira ya joto pale uchumi utakapofikia kiwango cha chini kabisa na kuanza kutulia kama wengi wanavyotazamia.

Hakuna sababu ya kuondosha kabisa kiwango cha riba kama zilivyofanya Marekani na Japan.Kwani mfuriko wa pesa unaweza kuathiri maendeleo ya kiuchumi. Masoko yakifurika na pesa zilizopatikana kwa mikopo rahisi,basi ni vigumu pia kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa na mara, utulivu wa masoko na ukuaji wa uchumi huingia hatarini. Kwani miongoni mwa mambo yaliyosababisha mzozo wa hivi sasa duniani,ni uoga wa taasisi za fedha nchini Marekani kuchukua haraka hatua za kukomesha sera za mikopo rahisi na sheria za uzembe katika masoko ya fedha nchini humo.