1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benitez ndiye kocha mpya wa Newcastle

11 Machi 2016

Klabu ya ligi Kuu ya England - Premier League - Newcastle United imempa majukumu ya ukufunzi Mhispania Rafael Benitez baada ya kumpiga kalamu Steve McLaren, ambaye alikuwa kocha mkuu kwa kipindi cha miezi tisa iliyopita

https://p.dw.com/p/1IBsz
Rafa Benitez Trainer Real Madrid
Picha: picture-alliance/dpa/B. Alino

Benitez mwenye umri wa miaka 55, kocha wa zamani wa Liverpool na Real Madrid, ana michuano kumi pekee kuidumisha hadhi ya Newcastle katika Premier League huku moja ya michuano hiyo ikiwa dhidi ya viongozi wa ligi Leicester City Jumatatu ijayo.

Taarifa ya Newcastle imesema Benitez ambaye alishinda Kombe la Europa akiwa kaimu kocha wa Chelsea, amesaini mkataba wa awali wa miaka mitatu. Amewaleta makocha wasaidizi Fabio Pecchia, Francisco de Miguel Moreno na Antonio Gomez Perez.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Gakuba Daniel