BEMBA to be transferred to ICC. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

BEMBA to be transferred to ICC.

Aliekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yumo njiani kufikishwa mbele ya mahakama ya mjini the Hague,ICC

default

Aliekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

BRUSSELS.

Mahakama ya Ubelgiji imeondoa vipingamizi vyote ili kuwezesha aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini J.K ya Kongo, Jean Pierre Bemba kupelekwa mjini the Hague kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita. Mahakama kuu ya Ubelgiji imepinga madai yaliyotolewa na mawakili wa Bemba kwamba taratibu za kisheria zilizofuatia ,baada ya kukamatwa kwake mjini Brussels mnamo mwezi mei hazikuwa sahihi.

Hatua ya kumpeleka Bemba kwenye mahakama ya kimataifa inayopambana na uhalifu ,ICC mjini the Hague ilikuwa inasubiri uamuzi wa mahakama.

Uamuzi huo unatarajiwa kutekelezwa karibuni.

Bemba alikamatwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels mwezi mei kufuatia hati ya kisheria ya mahakama ya kimataifa ya ICC. Anakabiliwa na mashtaka manne ya uhalifu wa kivita na mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu anayodaiwa kutenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 • Tarehe 02.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EUY2
 • Tarehe 02.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EUY2
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com