Bellarabi aitwa katika timu ya Ujerumani | Michezo | DW | 03.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bellarabi aitwa katika timu ya Ujerumani

Mshambuliaji wa kulia wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi amechaguliwa katika timu ya taifa ya Ujerumani. Mchezo mzuri wa Max Kruse msimu huu pia umempa tikiti ya kujumuishwa katika kikosi cha taifa.

Bellarabi ameitwa katika timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza kwa ajili ya mechi mbili za mwezi huu dhidi ya Poland na Jamhuri ya Ireland.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu katika ligi ya taifa baada ya kumaliza msimu uliopita katika klabu iliyoshushwa ngazi ya Eintracht Braunschweig kwa mkataba wa mkopo. Chini ya kocha mpya Rodger Schmidt, Bellarabi amefunga magoli mawili katika mechi zake sita za kwanza, na kuwaandalia wenzake magoli matatu ya Leverkusen kwenye ligi ya Ujerumani.

Max Kruse wa Borussia Mönchengladbach anarejea baada ya kuwa nje mechi kadhaa kutokana na jeraha. Bastian Schweinsteiger, Sami Khedira, Marco Reus na Mario Gomez wamewachwa nje ya mechi hizo mbili ambazo zitachezwa Octoba 11 na 14.

Kikosi kamili cha Ujerumani:

Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Borussia Dortmund), Matthias Ginter (Borussia Dortmund), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shrokdan Mustafi (Valencia), Antonio Rüdiger (Stuttgart), Sebastian Rudy (Hoffenheim)

Viungo: Karim Bellarabi (Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Toni Kroos (Real Madrid), Christoph Kramer (Gladbach), Thomas Müller (Bayern Munich), Mesut Özil (Arsenal), Lukas Podolski (Arsenal), Andre Schürrle (Chelsea)

Washambuliaji: Mario Götze (Bayern Munich), Max Kruse (Gladbach)

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu