1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE:Wajumbe kujadilia mustakabal wa Kosovo

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaU

Wajumbe wa Marekani,Umoja wa Ulaya na Urusi wanakutana na maafisa wa Serbia hii leo katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mazungumzo yaliyokwama kuhusu mustakabal wa Kosovo.Ziara hiyo ni ya kwanza tangu wasuluhishi wapya kukabidhiwa jukumu la kuendesha awamu ya kwanza ya mazungumzo kati ya Serbia na Kosovo.Mjumbe wa Marekani Frank Wisner,Wolfgang Ischinger wa Umoja wa Ulaya vilevile Alexander Botsan-Kharchenko wa Urusi wnaakutana na Rais wa Serbia Boris Tadic, akiwemo Waziri Mkuu Vojislav Kostunica pamoja na maafisa wa ngazi za juu.

Kosovo ni sehemu ya Serbia ila wakazi wake wengi wana asili ya Albania na kudai uhuru kamili wa kujitawala.Dai hilo linakataliwa na Serbia na Urusi iliyo na kura ya turufu kuhusu suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kosovo imekuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 99.Kwa mujibu wa mjumbe wa Umoja wa Ulaya mkutano huo hauazimii kutoa mapendekezo mapya kwani mpango uliowasilishwa na mjumbe wa zamani wa Umoja wa mataifa Marrti Ahtisaari ndio unaofatwa.