1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belgrade. Kosovo kutangaza uhuru.

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBix

Viongozi wa jimbo la Kosovo wenye asili ya Albania wametoa ishara kuwa wanafikiria kutoa tangazo la pamoja la uhuru kutoka Serbia. Waziri wa mambo ya kigeni wa jimbo hilo kwa sasa veton Surroi amesema kuwa umoja wa mataifa hautoi tena njia kwa ajili ya uhuru kwasababu ya vipingamizi vinavyowekwa na Russia kwa niaba ya mshirika wake Serbia.

Surroi amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango A umeshindwa na kwamba muda umefika sasa kwa ajili ya mpango B.

Hali ya wasi wasi baina ya mataifa ya magharibi na Russia imekuwa ikiongezeka wiki hii kuhusiana na suala la Kosovo. Mataifa ya Ulaya na Marekani yanaunga mkono uhuru wa Kosovo wakati Russia inaunga mkono juhudi za Serbia kulibakiza jimbo hilo mikononi mwake.

Russia imesema wazi kuwa itatumia kura yake ya turufu dhidi ya azimio lolote la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu Kosovo ambalo halitatilia maanani kuhusu upinzani wa Serbia.