BELFAST:Mahasimu wa kisiasa wafikia muafaka wa kihistoria Ireland Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 27.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BELFAST:Mahasimu wa kisiasa wafikia muafaka wa kihistoria Ireland Kaskazini

Vyama viwili vikuu hasimu vya Protestant na Catholic, huko Ireland ya Kaskazini, hatimaye vimefikia makubaliano ya kihistoria, ya kuunda serikali ya pamoja ambayo itakuwa na mamlaka katika jimbo hilo la Uingereza.

Ian Paisley kiongozi wa chama cha Democrat Unionist na mwenziye Gerry Adams wa Sinn Fein, waliwaambia waandishi wa habari mjini Belfast ya kwamba makubaliano hayo yataanza rasmi utekelezaji wake tarehe 8 mwezi Mei.

Hiyo inafuatia mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya viongozi hao.Ian Paisley amekuwa akikataa kukutana uso kwa uso na viongozi wa Sinn Fein.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com